|
|
Kufyonza na Kunyonya
Date: 30 March 2004
- Si uwongo ni ya kweli, utadhani humo simo
Hufyonza kitu kikweli, hujaza tele mdomo
Meno hupotea mbali, ukadhania hayamo
Kinyonywacho huhimili, kikazama kwenye shimo
Maher Fundi
Kufyonza na Kunyonya
Date: 30 March 2004
- Tutawakhini wenzetu, watakosa ya muhimu
Elimu ni nuru yetu, haya sharti ufahamu
Situfiche tupe vitu, kama vipo tukirimu
Kwani kuna kipi kitu, kibaya kilo haramu ?
Maher Fundi
|