.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Nikuonavyo ni Hivi

 

 

 

 

 

 

Related links

Nikuonavyo ni Hivi!

Date:  01 April 2004

  1. Huna lako, umeishiwa zamani
    Kazi yako, kujipachika kundini
    Cheo chako, mekueka limbukeni
    Hivi ndivyo ulivyo
  2. Mekusoma, nikakujuwa undani
    Nimekoma, mwisho wetu mitaani
    Menichoma, donda mekaa moyoni
    Hivi ndivyo ulivyo
  3. Si kwa shari, haya ,nikukumbushayo
    Jihadhari, njia mbaya upitayo
    ,kivinjari, tafikwa na wayo wayo
    Hivi ndivyo ulivyo
  4. Ukiranja, kutaka paa angani
    Hu mjanja, kumshinda rahamani
    Kwa kiganja, utakuja rudi chini
    Hivi ndivyo ulivyo.

 

Ally (Yarabi Stara)

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet