.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

WEWE NI PUMZI ZAKE

 

Related links

WEWE NI PUMZI ZAKE

Date: 30 September, 2004

  1. Anahitaji mapenzi, na deko lako kupewa
    Kwa hanini umuenzi, roho ipate kutuwa
    Umpunguze majonzi, alonayo yasopowa
    Bila ya wewe hawezi, kuishi akawa sawa


  2. Wewe ni pumzi zake, uhai ulobakia
    Hana pengine ashike, kwako yeye maridhia
    Simuadhibu muweke, mwenzio anaumia
    Lizuwie chozi lake, asichukie dunia


  3. Tepe tepe hajiwezi, kesha umem'maliza
    Anasema wazi wazi, hafichi anatangaza
    Si maskhara hachezi, ndani yana muunguza
    Anachoomba ulezi, pendo lenu kulikuza

Maher Fundi

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet