Ra – Rabbi tutunuku toba
Ma – Maghufira kwa viroba
Dha – Dhambi mchongoma miba
Ni – Ni’ima iso na riba
RAMADHANI, MWEZI WA HAIBA
Sa – Sala ni zaka ya mja
U – Uja kukiri Mmoja
Mu – Muumba wa wote waja
SAUMU, KITO CHA FADHILA
Ta – Tabasamu la furaha
Ra – Rabbi ametupa siha
We - Wengi nyoyo zina raha
He – Hekima za Mwenye Jaha
TARAWEHE, SUNA KUTOKA KWA BWANA
La – Lala kidogo mumini
I – Ibada kithirisheni
La – La kheri kimbilieni
Tu – Tunzo toka kwa Manani
L’ – L’haqu tuabuduni
Qa – Qadiru muogopeni
D’ – Dini tupiganieni
Ri – Riziki tushukuruni
LAILATUL QADRI, NEEMA ISO KIFANI
Ahmed Rashid.