|
|
Yanayo Tuudhi Kuyaona
Date: 23 May 2004
- Kwani lipi la muhimu, lazima tulikubali
Kwa unayo tutuhumu, ikawa kubwa shauri
Tumeridhika yadumu, kwetu harufu nzuri
Huyapendi,hunahamu, nenda bara kuno kheri
- Mtu kwao hujisifu, nami naona fakhari
Visiwa vyetu nadhifu, kwa mila na desturi
Iweje useme chafu, nasi tupige muhuri
Ulinganishe harufu, ya kambare na bukhuri!
Maher Fundi
|