.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

BIBI NA BWANA

 

 

 

 

 

 

Related links

BIBI NA BWANA

Date:  30 March 2004

  1. Furaha furaha sana, furaha bibi na bwana
    Ni ambari na zinduna, mapenzi mulovishana
    Mikono mukishikana, munapendeza vijana
    Mushakamilisha suna, kwa baraka za Rabana

  2. Nyoyo mukisafiana, mazuri kuambizana
    Siri zenu kuzibana, na bashasha kupeana
    Pia kusubiriana, kosa kusameheana
    Mutazishinda fitina, mutazidi kupendana

  3. Muzidi kufungamana, kwa raha kunyunyizana
    Muruzukiwe na wana, waume kwa wasichana
    Muishi kusikizana, penye shida au ghina
    Hadi kukhitimishana, peponi mwende kutana

KIITIKIO

Furaha bibi na bwana, mushakamilisha suna
Ni ambari na zinduna, mapenzi mulovishana

SHAIRI : SALEH M. BARKEY

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004-2006 Zanzinet