.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Kiumbe Hasarifiki

 

 

 

 

 

 

Related links

KIUMBE HASARIFIKI

Date:  23 January, 2005

  1. Huyo kachanganyikiwa, hana mbele hana nyuma
    Mwenyewe nguo kavuwa, kwenye hadhara ya umma
    Kaishiwa kachachiwa, namuonea huruma
    Achekwa akejeliwa, kila akijitutuma

  2. Azurura kila njia, mambo yamemsakama
    Asumbuka na dunia, wateja wamemhama
    Apita kukamatia, aibu mji mzima
    Muflisi wa tabia, kila mtu amsema

  3. Alipopewa shubiri, yeye kachukua pima
    Alijidhani hodari, kutamba na kunguruma
    Kumbe watu wamnyari, kimya wanamtazama
    Keshamaliza safari, amekwisha kadi tama

  4. Kiumbe hasarifiki, Wallahi bora mnyama
    Ni thakili habebeki, saliti wa kila jema
    Makuhuluki mnafiki, mwishowe hana salama
    Stahili mzandiki, radhi zinamuandama

KIITIKIO
Kiumbe hasarifiki, saliti wa kila jema
Jaza yake mzandiki, radhi zinamuandama


Shairi: Saleh Barkey - 16th August, 1997

Limeletwa na unique

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet