.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Mwisho Nimefika

 

 

 

 

 

 

Related links

                   

Date: 13 December, 2005

Kwa wale wapenzi wa sanaa hii ya urari wa vina, na muwala wa beti na mishororo y! ake, huu ni utungo wa kiroho na kimaanawi. Tafadhalini natuusome kwa kituo.
                                          ************
                                            
                                   MWISHO NIMEFIKA
 
Mwangi unagonga, sikioni mwangu, mja kuniita, natika labeka.
Yule anopanga, kunondoa pingu, kutoa utata, nuru nawirika.
Kaja njiwa manga, zanawiri mbingu, kheri kuipata, kuusha mashaka
Ni Allah wangu Rabuka.
 
Kaondoa wingu, akili burudi, twabiki fiili, ndipo taokoka
Busitani yangu, kajaza waridi, nazo mbawa mbili, kanipa Rabuka
Udhaifu wangu, mkubwa shitadi, kanipa akili, iwe kuongoka
Ni nani Wako mithili?
 
Kanifunza panda, paa uenende, fika kileleni, twii Mtukuka
Ni wangu uwanda, napepea nende, Kwake Rahmani, nifike haraka
Nechoka kuranda, nemaliza konde, hikwama kingoni, mwisho nimefika
Kwa Nuru yangu samawi.
 
Nalijidanganya, hajipurapura, nikajipumbaza, eti sina shaka
Yakanikanganya, kuniparapara, yakanichakaza, nikafadhaika
Mja kunifinya, dunia tambara, limeniburuza, yameshanifika
Mwokozi unasi ameniokoa.
 
Nyuma sendi tena, Kwake nimesaki, sikutaki tena, dunia mashaka
Niko hai tena, ni kwa Mmiliki, moyo sifi tena, nimeshaokoka
Sinache Rabbana, mja tahiliki, nekusaka sana, mwisho nimefika
Ni Wewe tu Rabbuka.
                                                  ************
Ahmed Rashid
  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet