.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Nakutafuta uliko

 

 

 

 

 

 

Related links

Nakutafuta uliko

Date:  08 March 2005

  1. Ndege wangu ndege wangu, nakutafuta uliko
    Nakuapia kwa mungu, moyo wangu uko kwako
    Sinipe kizungu zungu, kunitangisha mwenzako
    Nakuhitajia kwangu, Nizipate raha zako

  2. Memaliza ulimwengu, sijapata fani yako
    Nimeipanda mikungu, kitizama kama uko
    Macho mefanya kiwingu, hayaoni kwengineko
    Urudi kipenzi changu, unienzi niwe wako

  3. Sisikize walimwengu, kutupa mahali pako
    Siharibu pendo langu, urudi hapa niliko
    Nikuenzi mboni zangu, ukijue cheo chako
    Nawangiwe na machungu, moyo mesabili kwako

  4. Mewapiku kwa mizungu, turufu zote ni zako
    Niradhi nitiwe pingu, sirudi nyuma mwenzako
    Rejea nyumbani kwangu, nichezee mbawa zako
    Wewe ndie ndege wangu, simtafuti mwenzako

Miminae

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet