.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Shume Linaunguruma

 

 

 

 

 

 

Related links

Shume Linaunguruma

Date: 20 October, 2005

  1. Si kicheko si kilio, nafusi i hamkani
    Siyajui majilio, hatima i kwa Manani
    Siujui muishio, ni yepi yalo usoni
    Shume linaunguruma, jama nilifanye nini?

  2. Nilitoe guniani, lejendee vichakani?
    Nilitie kitanzini, lienende kuzimuni?
    Nilikongowe kwapani, life likitumaini?
    Shume linaunguruma, jama nilifanye nini?

  3. Limekubuhu kwa wizi, masinzi tele usoni
    Limewashinda wazazi, nakama kwa majirani
    Limemaliza viunzi, hamkaliki nyumbani
    Shume linaunguruma, jama nilifanye nini?

Ahmed Rashid

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet