|
|
Chozi!
Date: 17 June, 2006
- Ewe chozi , endelea kudondoka
Yako enzi, imekawia kufika
Mpanda ngazi , amekataa kushuka
Nimeshindwa mie
- Yangu dhana , yakuwa yatageuka
sina tena , tamaa imezimika
haya hana , ashindana na rabuka
Nimeshindwa mie
- Ana hanja , madhila kukupachika
Si mjanja , Ila amelaanika
Anavunja , Hapo anonufaika
Nimeshindwa mie
- Wewe ona , moyoni yakuumize
Ukipona , katu yasikupendeze
Kweli nena , mabwana uwachukize
Yangu leo sio kesho yako
Said Paul
|