|
|
HUNA SUMILE!
Date: 22 June, 2006
- Wendavyo huna sumile, huyajali ya njiani
Vikwaruzavyo vitele, waona hujulikani
Huchwi kufungwa kengele, masikini wa rohoni
Siwatajii mchawi , mfumbuweni fumboni
- Ulopewa ni shubiri, pima yakuhusu nini
Ukatamba una ari, umeushika mpini
Waona umevinjari, kumbe uko ukutini
Simfichui mchawi, mtambuweni fumboni
- Ngoma hiyo ya kitoto, haikeshi asilani
Kujipulizia joto, raha yake raha gani
Umejitweka mazito, kwa kutaka ubishani
Mchawi hasemwi jina , nawatajia fumboni
Saleh Barkey
|