.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Kipigo kwake sawia!

 

 

 

 

 

 

Related links

Kipigo kwake sawia!

Date: 17 July, 2006

  1. Atukanaye mamako, sawia kwake kipigo
    Kwa kichwa au kiboko, mradi kiwe kipigo
    Kama mwizi kwenye soko, tumia hata muhogo
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako

  2. Mfano bora Zidani, kutoa hicho kipigo
    Tusi kwa mama la nini?, onyo la kweli kipigo
    Ajifanyaye muhuni, komesha yake kipigo
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako

  3. Hutuzwa mcheza kwao, ukitowapo kipigo
    Mfate hata makwao, masaki au kigogo
    Hata alie kikwao, mpige japo kidogo
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako

  4. Kipigo kwake sawia, nasema sifanyi zogo
    Wajibu nawaambia, kukitembeza kipigo
    Ataijuwa dunia, akipatapo kisago
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako
  5. Nasema kweli halali, kitolewapo kipigo
    Tena mamako mjali, tembeza hicho kipigo
    Mpige japo kwa mbali, ajue nawe ni mbogo
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako
  6. Nafika hapa tamati , msisahau kipigo
    Msiogope kamati, kutoa hicho kipigo
    Karati au manati, ili mradi kipigo
    Sawia kwake kipigo, atukanaye mamako

Msanif Shaaban K.

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004-2006 Zanzinet