|
|
BAADA YA BUTIAMA!
Date: 02 April, 2008
- Bwana Ramadhani Juma,
Umenituma,
Bila ya tuhuma
- Mjini kwa Wasukuma,
Wenye kufuma,
Tamaa za Umma
- Nende na wako utumwa,
Wenye huruma,
Kwa wenye huduma!
- Siwezi hata kidogo,
Penye vigogo,
Wa hivyo visogo
- Kukurubia padogo,
Bila ya hongo,
Kwa yao mikogo
- Nami sitokwenda Bongo,
Mtaa wa Congo,
Nikanywishwe gongo!
Salim Himidi
|