|
|
HAKUNA MWAFAKA!
Date: 24 April, 2008
- Wa Funguni umechochea
Kufanya sote tutete
Usemayo hutokea
Kwa wetu huyu Kikwete
Mwanadamu hukosea
Kumbuka walio WETE!
- Kumbuka walio Wete
Na hata huko PUJINI
Mkamandume tesa tese
Fimbo "Arba Arbaini"
Si hoja mpweke foke
Bora tuketi MAKINI!
- Bora kuketi makini
Tuhifadhi mba chao
Tusende Mfenesini
Mchanga mavumbi KWATO
Tuelewe kwa yakini
Haki zetu ziko kwao!
- Haki zetu kuwa kwao
Tutathmini nguvu zetu
Kuandama watu hawo
Si unyago huko kwetu
Mtu hucheza kwao
Hayo tujuwe, wenzetu!
- Hayo kujuwa, wenzetu
Vizuri, mbinu kugawa
Tuthamini Ndugu Sefu
Muongozi wa BUSARA
Yuwajua yalo yetu
Hayo msiwe WAHARA!
Salim Himidi
|