.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

HEKO DA SALMA!

 

 

 

 

 

 

Related links

HEKO DA SALMA!

Date: 15 April, 2008

  1. Kadhia hii ni nzito, yenza aibu na ufinyu
    Wala si sera ya mpito, ni ya itikadi na mbinu
    Wajib kuipangua vito, kwa kuhifadhi chetu kinu!

  2. Na kuhifadhi chetu kinu, ni kujitwangia maana
    Tusiige ya wenye ZANU, yao Zimbabwe kuichana
    Hata tufikapo ONU, kwa viongozi kusutana!

  3. Na viongozi kusutana, ndio kheri ya kwetu sote
    Kusimamisha mahakama, pa hayo kuyasema yote
    Waungwana hawato zama, kwa kuto ogopa chochote!

  4. Kwa kuto ogopa chochote, na kufunuwa kwa makini
    Uwongo ufichuke kote, majabari wanapo khini
    Na ukweli usi kokote, pale wakatapo maini!

  5. Pale wakatapo maini, ni pa kuvunja wetu moyo
    Tusionee masikini, kuvumilia wenye choyo
    Tusijitose baharini, kwa kuridhisha Bagamoyo!

  6. Kwa kuridhisha Bagamoyo, Wapemba waona mazito
    Hawatokwenda kamwe Tokyo, na katafuta ya mpito
    Kwani wao si mabogoyo, wa kutafuna hivyo vito!
  7. Salam Bi Salma salamu, ama kweli wanikosha
    Kwa wako mshiko kalamu, maelezo kuyaanyosha
    Na lugha lako timamu, wajinga kuwapotosha!

  8. Wajinga kuwapotosha, ni kutunuwa matende
    Twende zetu Kigomasha, nduzetu tuwapende
    Kwa fahari na tamasha, na sio kwa peremende!

  9. Na sio kwa peremende, kwani wao si mikizi
    Wa kusuma twende, ni wa kuzamia mbizi
    Kwenye milima na mabonde, na kuandama mabwizi!

  10. Na kuandama mabwizi, ni kusafisha wetu moyo
    Kwa vituko vya siku hizi, kutawalisha wenye choyo
    Wa zuwao ukimbizi, kutuhamisha Bagamoyo!

  11. Kutuhamisha Bagamoyo, ni kutufukuza makwetu
    Kutufanya watu ovyo, na kupora mali zetu
    Katu tusikubali hayo, shime vijana wetu!

Salim Himidi

HEKO DA SALMA!

Date: 17 April, 2008

  1. Shekh Salim mtunzi, nishani ninakutunza
    Mwenzetu unaujuzi, hakuna anokuweza
    Kijiweni kuna kazi, tutumie mbinu pweza.

Hashil Seif

HEKO DA SALMA!

Date: 17 April, 2008

  1. Maalim umetamani, hii nishani kunitunza
    Mi si mtu wa thamani, kwa yote ulonifunza
    Elimu ya Makuhani, ya Janab kukujaza!

  2. Na Janab kukujuza, hajajua haya yote
    Ndo wivu wa Mke Mwenza, kuangamiza mila zote
    Wazanzibari kutomeza, haluli ya nduli zote!

  3. Haluli ya nduli zote, imetia bawasili
    Kuvunja kunga zote, kwa kupoteza akili
    Na watwani si cho chote, duniani leo hii!
  4. Duniani leo hii, kutambua mtu kwao
    Adhabu ya Wahshii, asojua lake jambo
    Si wa Dola si wa Ntii, huko Ndani hata Ngambo!
  5. Huko Ndani hata Ngambo, hutambui kipi chetu
    Hiyo Mbiu Ya Mgambo, na hizo haki zetu
    Hazina tena majambo, yako wewe na Sepetu!

Salim Himidi

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet