.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

MJUE PROF. MAZRUI!

 

 

 

 

 

 

Related links

MJUE PROF. MAZRUI!

Date: 08 April, 2008

  1. Mpitanjia sbalkheri, wala wewe si Mnyonge
    Subira huvuta kheri, kwa kuja na lako tonge
    Mazrui msema kweli, kwetu Mjini na Donge!

  2. Kwetu Mjini na Donge, tafuta wa kutwambia
    Situletee mikonge, ya kuharibu tabia
    Kwani sisi si vishonde, kunajisi Hamzia!

  3. Kunajisi Hamzia, mambo hayo si ya kwetu
    Kote tunakoingia, husafisha nia zetu
    Wala hujayasikia, katika Ukumbi wetu!

  4. Na Wanaukumbi wetu, si watu walona choyo
    Kujua ndo kipi chetu, ni haki yetu ya moyo
    Tumehifadhi Sepetu, Unguja na Bagamoyo!

Salim Himidi

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet