|
|
MWAFAKA KUKOMAA!
Date: 02 April, 2008
- Maalim umenyamaa, na sote tumeduwaa
Muwafaka kukomaa, Kafu kakosa jamaa!
- Lakini hiyo tamaa, imeshatowa balaa
Kwa Kenya kwisha kupaa, Zimbabwe hazijafaa!
- Mkaidi si shujaa, wala nguo hatovaa
Ajigamba kama kaa, tena hana pakukaa!
- Amani si majukwaa, wala Salama si njaa
Subira kweli hufaa, lakini kwa mwenza haya!
Salim Himidi
|