.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

NA SISI TUMECHOKA!

 

 

 

 

 

 

Related links

NA SISI TUMECHOKA!

Date: 02 April, 2008

  1. Nakupa yangu pongezi, Abuu Shani kutujuvya
    Mawazo yako mapenzi, Zenjibari kutukuka!

  2. Kwa haya uliyosema, yatupasa kukwambia
    Ni ya wingi wa rehema, kwa wakati kuwadia!

  3. Na hakika umeona, pa ukweli kupangia
    Sefu naaje kushona, yake nguo kuchangia!

  4. Salimini atapona, macho yake kutangia
    Pale Jumbe aliona, imani kumjilia!

  5. Mwinyi pia ana kona, ya mpira kupigia
    Na Bilali hatofonya, kwenye kheri kuingia!

  6. Haya maneno kutona, si mazito kusikia
    Ni yetu sote kuponya, kuchanganya zetu nia!

Salim Himidi

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet