|
|
NISHANI KUMTUNZA!
Date: 17 April, 2008
Shekh Salim mtunzi, nishani ninakutunza
Mwenzetu unaujuzi, hakuna anokuweza
Kijiweni kuna kazi, tutumie mbinu pweza.
Hashil Seif
Date: 17 April, 2008
- Maalim umetamani
Hii nishani kunitunza
Mi si mtu wa thamani
Kwa yote ulonifunza
Elimu ya Makuhani
Ya Janab kukujaza!
- Na Janab kukujuza
Hajajua haya yote
Ndo wivu wa Mke Mwenza
Kuangamiza mila zote
Wazanzibari kutomeza
Haluli ya nduli zote!
- Haluli ya nduli zote
Imetia bawasili
Kuvunja kunga zote
Kwa kupoteza akili
Na watwani si cho chote
Duniani leo hii!
- Duniani leo hii
Kutambua mtu kwao
Adhabu ya Wahshii
Asojua lake jambo
Si wa Dola si wa Ntii
Huko Ndani hata Ngambo!
- Huko Ndani hata Ngambo
Hutambui kipi chetu
Hiyo Mbiu Ya Mgambo
Na hizo haki zetu
Hazina tena majambo
Yako wewe na Sepetu!
Salim Himidi
|