.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

SIULUMBI MULUMBAO!

 

 

 

 

 

 

Related links

SIULUMBI MULUMBAO!

Date:  09 January, 2008

  1. Ndimi mgeni wa Numbi, mwenyeji kale 創okuwa
    Nijili kwenu waambi, kuzinga la kuambiwa
    Bali hakuta ulumbi, nami ukanishituwa
    Na nilipouchunguwa, haona ni wa vitimbi.

  2. Ging段ngi ya Waging段ngi, si ya miye mtolewa
    Nami nacha nena mengi, bawabu akanitowa
    Lakini hayanitwangi, maneno yanotumiwa
    Kulumbana kwa vifuwa, si ulumbi wa Ging段ngi.

  3. Waging段ngi kwa ulumbi, ni kazi yenu najuwa
    Bali sio ujigambi, wa wengine kuumbuwa
    Kwamba mtamba hatambi, asikucha kutambiwa
    Mbona nyie mwacheuwa, au mushashiba tumbi?

  4. Nasi tuli Waging段ngi, wa kutolewa vikowa
    Tukalumbana kwa mingi, bali lugha twechaguwa
    Mbona nyie hamutungi, mwaumba mukiumbuwa?
    Kwa hivi munabomowa, ndugu zangu hamujengi.

  5. Lau kweli mu walumbi, lumbanani kwa satuwa
    Musilumbane kwa kambi, na pande pande mukawa
    Agambapo mjigambi, ujuwe hajajijuwa
    Kwamba lau ajijuwa, mwenye gambo hajigambi.

  6. La urongo silirongi, madharaye nayajuwa
    Nawe ola Mging段ngi, 壮ingoje ukalolewa
    Kwamba zipo siku nyingi, zako weye hapa kuwa
    Vipi ulomshushuwa, akaja kuwa ni mwingi?

  7. Ulumbi wa ujigambi, na kujipiga kifuwa
    Mlangoni pa Ging段ngi, si jambo la kusifiwa
    Uonwe kuwa ni dhambi, na kharamu yenye dowa
    Nami ninawazinduwa, mukome huu ulumbi!

Mohammed Ghassani

SIULUMBI MULUMBAO!

Date:  10 January, 2008

  1. Al Akhi mshairi , baswiri muona mambo
    Katu si yangu dhamiri , kukupiga kwa vikumbo
    Uliyonena hariri , tuyatakayo kitambo
    Wagange watagangika , Gin'gingi nawe ni mwako

  2. Nduguyo akinaswa , kwa fitina kuwa chambo
    Huraiwa na kuaswa , asizidi kwenda kombo
    Kuongozwa si kukoswa , nasaha ni chema chombo
    Wagange watagangika , Gin'gingi nawe ni mwako

  3. Walumbao yasolumbwa , watuumiza matumbo
    Awali ndivyo kuombwa , kutaradhiwa kwa nyimbo
    Mwishowe sawa kugombwa , washikiwe hata fimbo
    Wagange watagangika , Gin'gingi nawe ni mwako

Saleh M. Barkey

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet