|
|
WAPINZANI WATOKA BUNGENI!
Date: 10 April, 2008
- Maalim wangu Hashili, Kinara fundi mwanana
Mawazo yako kukiri, ni fimbo ya Subuhana
Yenye wingi wa akili, kwa marefu na upana!
- Kwa marefu na upana, lazimu wewe utete
Wala si kwa kutukana, hayo sio ya upweke
Watapowafikiana, Zanzibar kwenda kidete!
- Zanzibar kwenda kidete, ni mambo kuyafahamu
Mfunga watu Kikwete, yadhibiti mahakimu
Tusije kuwa viwete, kushindwa na mabuhamu!
- Kushindwa na mabuhamu, ni sawa na kwendwa choo
Vinyama na wanadamu, sote wana wa kondoo
Tumuandame kwa hamu, Kubeli la Bagamoyo!
- Kubeli la Bagamoyo, ndie mwenye kukithiri
Amali za matokeo, kupunguza pilipili
Mapenzi yetu ya leo, yatupasa tufikiri!
Salim Himidi
|