.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

BASAKHERA

 

 

 

 

 

 

Related links

BASAKHERA

Date:  28 January, 2005

  1. Muongo Basakhera muongo tena Basakhera muongo
    Kuna kijti kimoja kikastawisha jengo
    Kuna pau kuna ndinga kuna n'gongo
    Nenda ukakate miti nije nikuonye jengo

  2. Paka nakukanya, usirambe tui
    Ungajinyon'gonya, maji huyajui
    Kama huli panya, na wali hupewi - jamani

  3. Chimbua choogo, chambo kiwe chingi
    Upate chachuo, na kamba wa lungi
    Jamani jongoo, hatuwi mtungi

  4. Nna mateso mwanamke nna mateso
    Mkajipamba vitambi, mkajitia na leso
    Akhera kuna mambo kesho

  5. Kanzu yashitaki, qadhi niamua
    Mimi sivaliki, mbona navaliwa
    Nimeoza dhiki, na pa kukaliwa
  6. Kofia nyekundu, imenipendeza
    Unga rorarora, macho makengeza
    Huachi mahana, ngoma ukacheza

Imeletwa na Saleh Barkey
Muimbaji : Mbaruku bin Talassam
enzi za Sitti bint Saad

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet