KAGHANI MWIMBAJI
Date: 03 March, 2005
Kaghani mwimbaji wa msafara sikiza
Kwa jina lataji la mtume mpendeza
Ngamia mwendani maumbile akicheza
Kwa ulevi wake kutajiwa mfaraji
Mtume: Kwa ulevi wake kutajiwa mfaraji
Rasuli: Kwa ulevi wake kutajiwa mfaraji
Habiby: Kwa ulevi wake kutajiwa mfaraji
Litazame kuba lenye rangi ya kibichi
Mtume sahiba yumo humo hajifichi
Nuru ya ghaiba anga lake la kila nchi
Liloondosha giza likatufaraji
Mtume: Liloondosha giza likatufaraji
Rasuli: Liloondosha giza likatufaraji
Habiby: Liloondosha giza likatufaraji
Yambie nafsi ondoka tena zungumza
Itoke upesi iwe na kujiliwaza
Isitie hisi hapana la kukukataza
Kwa muhibu wako nena unalotaraji
Mtume: Kwa muhibu wako nena unalotaraji
Rasuli: Kwa muhibu wako nena unalotaraji
Habiby: Kwa muhibu wako nena unalotaraji
Mtume wa Mungu Bwana wa viumbe pia
Mtukufu tangu na cheo kilotimia
Daraja kichungu Mola amemjazia
Kila la ubora amepewa mfaraji
Mtume: Kila la ubora amepewa mfaraji
Rasuli: Kila la ubora amepewa mfaraji
Habiby: Kila la ubora amepewa mfaraji
Lau tungekwenda Madina kwa siku zote
Bila ya kupanda ngamia au chochote
Ila twampenda mtume dunia yote
Ingali tupasa kufika kwa mfaraji
Mtume: Ingali tupasa kufika kwa mfaraji
Rasuli: Ingali tupasa kufika kwa mfaraji
Habiby: Ingali tupasa kufika kwa mfaraji
Lau twafanza kila mara maulidi
Yakumtukuza tumwa wetu Muhammadi
Muondosha giza mpenzi wa Mola Wadudi
Ingali tupasa kumsifu mfaraji
Mtume: Ingali tupasa kumsifu mfaraji
Rasuli: Ingali tupasa kumsifu mfaraji
Habiby: Ingali tupasa kumsifu mfaraji
Mola mchunguzi mpelekee rehema
Tumwa muokozi nyakati zote daima
Zende wazi wazi kwa mtume wetu hashima
Atae simama kutuvusha mfaraji
Mtume: Atae simama kutuvusha mfaraji
Rasuli: Atae simama kutuvusha mfaraji
Habiby: Atae simama kutuvusha mfaraji
Ali na sahaba na wote wapelekea
Na walo ibeba haki kufata sharia
Tunataka toba mtume kutusimamia
Kuombea kwako Mola atatufaraji
Mtume: Kuombea kwako mola atatufaraji
Rasuli: Kuombea kwako mola atatufaraji
Habiby: Kuombea kwako mola atatufaraji
Salallahu ala Muhammad, Salallahu alyh wasalim
Imeletwa na Anonymous