.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Madaraka Yana Mwisho!

 

 

 

 

 

 

Related links

Madaraka Yana Mwisho !

Date:  06 January, 2007

  1. Kwa jina lake manane, Mola mwenye upendo,
    Asokua na khiyana, sifa zake ni mrundo,
    Mwana Adam ni dhaifu, usijifanye komando,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  2. Salmin ulitamba, kwamba wewe ni kombando,
    Sasa muda umekwisha, umebaki ni kondoo,
    Umekuwa kama kuku, aloshikwa na mdondo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  3. Zanzibar kama yako, ulishika kwa kishindo,
    Wenzio unawatesa, gerezani kwa marundo,
    Watu tulikirahika, kwa maneno ya uvundo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  4. Pemba walikukataa, mavi ukanya mrundo,
    Maji ukayachafua, watu wakenda kando,
    Ukajifanya kifaru, hakuna tena upendo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  5. Ukajifanya kafiri, Mungu kumuweka kando,
    Sasa leo kiko wapi, umechezeshwa msondo,
    Na bado kesho Akhera, utakipata kipondo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  6. Madhila uliyofanya, wewe ukaona bado,
    Muda wataka ongeza, utufanyie kishindo,
    CCM namba moja, wakakupiga kwa nyundo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.
  7. Ndugu zako wawatesa, kuwapiga kwa upondo, Sheria ukaipinda, kama nguo ya upindo, Wenzio wakakupamba, kwamba wewe ni komando, Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

  8. Sasa ujirekebishe unavyokwenda si mwendo,
    Mimi ninae kuonya, ninaitwa Mwela Bondo,
    Sikama nakusimanga, ninaondoa mfundo,
    Madaraka yana mwisho, usiwe mwenye kiburi.

Limeletwa na Abdalla Sani

Mtungaji : Mwela Bondo (Kipupwe), Makumbusho, Dar es Salaam

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet