Zanzinet Self Services
ZANZINET Self Service ni huduma inayomuezesha mjumbe wa Zanzinet kujiondoa kwenye ukumbi (Unsubscribe), kuzuia kupokea barua kwa muda (Set Nomail), na huduma nyenginezo zinazohusu uanachama wa mjumbe kwenye ukumbi huu.
Kujiondoa Zanzinet:
Kama unataka kujiondoa kabisa kutoka kwenye Zanzinet, andika anwani yako ya email kwenye sehemu zilizoainishwa na baada ya kubonyeza kifungo cha "BONYEZA HAPA" kilichopo hapa chini, andika "password" yako chini ya sehemu ya "Unsubscribing from Zanzinet" na baadaye bonyeza kifungo cha "Unsubscribe".
Je, hupati kitu kutoka ZANZINET?
Kama hupati kitu kutoka Zanzinet, andika anwani yako ya email kwenye sehemu zilizoainishwa na baadae ubonyeze kifungo cha "BONYEZA HAPA" kilicho hapa chini.
Kwenye ukurasa utakaotokezea angalia sehemu ya "Your Zanzinet Subscription Options". Chini ya "Disable mail delivery" angalia kama imechaguliwa "On" wewe chagua "Off" kisha andika "password" yako na ubonyeze "Submit My Changes". Kama huijui "password" yako bonyeza sehemu yenye maneno "Email My Password To Me". Ukifanya hivyo utapelekewa "password" yako kwa njia ya email. Ukiipata itumie kama ilivyoelekezwa hapo juu.
Kusimamisha kwa muda barua za ZANZINET:
Kama unataka kusimamisha kwa muda barua za Zanzinet, andika anwani yako ya email kwenye sehemu zilizoainishwa na baadae ubonyeze kifungo cha "BONYEZA HAPA" kilicho hapa chini.
Kwenye ukurasa utakaotokezea angalia sehemu ya "Your Zanzinet Subscription Options". Chini ya "Disable mail delivery" angalia kama imechaguliwa "Off" wewe chagua "On" kisha andika "password" yako na ubonyeze "Submit My Changes". Kama huijui "password" yako bonyeza sehemu yenye maneno "Email My Password To Me". Ukifanya hivyo utapelekewa "password" yako kwa njia ya email. Ukiipata itumie kama ilivyoelekezwa hapo juu.

